Tafuta katika Blogu Hii

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EKILI ONE. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo EKILI ONE. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 13 Machi 2014

AIBU FAHAMU MAKAHABA WANAONGOZA KWA KUJIUZA MKOANI DODOMA...!!NOUMAA SANA..!

Na.Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya 21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP amewataja watu hao kuwa ni:

1. VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23, Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.
2. ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30, Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.

3. MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26, Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.

4. REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka 38, Mlugulu mkazi wa Airport Morogoro.

5.JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22, Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.

6. FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20, Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.

7. BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27, Mkurya mkazi wa Tarime Mara.

8. SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23, Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.

9. ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28, Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.
10. SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.

11. HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31, Mnyamwezi mkazi wa Urambo Tabora.

12. AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38, Mbulu mkazi wa Babati Manyara.

13.JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka 31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.

14.DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29, Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.

15.DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23, Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.
Aidha Kamanda MISIME amesema katika msako huo watu wawili wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane (8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.
Pia huko katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.
Kamanda MISIME amesema msako unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi

SAMWELI SITA AULA BUNGE LA KATIBA

Hatimaye Samweli Ameukwaa Uspika wa Bunge la katiba leo hii jioni kwa kwa kupata kura nyingi ....Mie Binafsi nimefurahi nahuhakika na Mzee huyo ...Kwani aliongoza Bunge Vizuri sana Enzi zake......Unasemaje kuhusu Sitta

LOWASSA AIKANA NOTI YA SH 500 YENYE PICHA YAKE BADALA YA RAIS.

Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.


Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi. Lowassa Amesema hajui na wala ahusiki na usambazaji wa Noti hiyo Mitandaoni

Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)

Jumamosi, 8 Februari 2014

WANA NCHI WA TABORA WATOA KERO ZAO JUU YA MAWASILIANO



WANANCHI wa kata za Loya na Lutende katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora wametoa kilio chao kwa  Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof  Makame Mbarawa, wakimwomba  kuwatatulia kero yao ya siku nyingi kwa kuwawekea mnara wa mawasiliano kwa ajili ya kupata huduma za simu za mkononi.

Kilio hicho wamekitoa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Igagula Dk Athuman Mfutakamba wakati wa ziara yake ya siku nne katika jimbo hilo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi pamoja na miradi mbali mbali ya maendeleo ya wananchi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wananchi hao wamesema kata hizo ni miongoni mwa kata ambazo hazina mawasiliano ya aina yeyote ile katika jimbo la Igalula kutokana na kutokuwa na mnara hata mmoja wa kuwasaidia kufanya mawasiliano hivyo kuwafanya wananchi hao kuwa nyuma kimaendeleo.

Wamebainisha kuwa kilio hicho cha kuomba kuwekewa minara kimekuwa ni cha siku nyingi na hakijapatiwa  ufumbuzi zaidi ya kupewa ahadi hewa mbunge wao  kila mara, hali inayowafanya baadhi yao kuichukia serikali ya chama cha mapinduzi kwa kuona kuwa haiwajali wananchi wake lakini kumbe wapi jamani.

Diwani wa kata ya Lutende Bwana Pancras Luge amesema Kilio cha wananchi wake ni mnara wa mawasiliano, na kwamba hapa hawawezi kuongea na simu hata kama kuna tukio la mauaji kama si kukanyaga baiskeli kwenda kutoa taarifa sehemu husika.

Luge amesema hivi sasa hawezi kupita barabarani kifua mbele kwani amekuwa akitukanuwa sana na wananchi kutokana na kukosekana kwa mawasiliano hayo ya Simu.

Akijibu tuhuma za wananchi dhidi yake  Mbunge wa Jimbo hilo Dk Athuman Mfutakamba amesema Serikali tayari imeshatenga fedha kwa ajili ya minara hiyo na mkandarasi tayari yupo na kuongeza kuwa yeye kama mbunge wao atafanya mawasiliano na Waziri anayehusika ili kuhakikisha wananchi wa Loya na Lutende wanapata mawasiliano ya simu za mkononi.

Nikiripoti kutoka wilaya ya Uyui mimi ni dikodiko.nyagale

JAMBAZI ARIYE KUWA AKIENDESHA MAUAJI MKOANI MAARA ATIWA MBARONI NA POLICE

Jambazi aliye itikisa tarime kwa mauaji ametiwa mikononi mwa police akiwa amekimbilia mkoani tanga
pia na mwenzake kuawa na jeshi la police kikosi cha kanda maalum akiwa ameachiwa bunduki aina ya Cmg
pia police wanaenderea na mahojiano zaidi ilikujua alikuwa analengo gani.