mwenga wetu
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani,Papa Francis amewalaumu wanandoa ambao wameamua kuishi bila kuwa na watoto, amesema uamuzi huo ni kitendo cha ubinafsi.
Papa alionya
utamaduni wa maisha bora yanayoweza kupatikana wakati wanandoa
wanapokuwa hawana watoto, lakini wana fedha za kutosha na kusema
inaonekana kuwa faraja ya kuwa na Mbwa, Paka na
kuwaonyesha mapenzi wanyama hao jambo ambalo sio sawa na baadaye ndoa
hiyo huishia kwenye uzee wenye uchungu na upweke mkubwa.
Kauli hiyo ilimechukuliwa kama changamoto kubwa Italia ambako kumeshuhudiwa kupungua kwa uzazi kwa kiwango kikubwa hivi sasa.
Papa amesema
jamii iliyoko katika kizazi kisichotaka kuzungukwa na watoto,
kinachowachukulia watoto kama chanzo cha shaka na matatizo ni jamii
iliyokubwa na msongo wa mawazo, kwani kuchagua kuto kuwa na watoto ni
ubinafsi, maisha huwa mazuri na kupata nguvu mpya kizazi
kinapoongezeka.