Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 17 Februari 2015

Maneno ya Papa Francis kwa wanandoa wasio na watoto..

mwenga wetu
Pope-Zuchetto_2766237bKiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani,Papa Francis amewalaumu wanandoa ambao wameamua kuishi bila kuwa na watoto, amesema uamuzi huo ni kitendo cha ubinafsi.
Kauli hiyo ilimechukuliwa kama changamoto kubwa Italia ambako kumeshuhudiwa kupungua kwa uzazi kwa kiwango kikubwa hivi sasa.
Papa amesema jamii iliyoko katika kizazi kisichotaka kuzungukwa na watoto, kinachowachukulia watoto kama chanzo cha shaka na matatizo ni jamii iliyokubwa na msongo wa mawazo, kwani kuchagua kuto kuwa na watoto ni ubinafsi, maisha huwa  mazuri na kupata nguvu mpya kizazi kinapoongezeka.
imagePapa alionya utamaduni wa maisha bora yanayoweza kupatikana wakati wanandoa wanapokuwa hawana watoto, lakini wana fedha za kutosha na kusema inaonekana kuwa faraja ya kuwa na MbwaPaka na kuwaonyesha mapenzi wanyama hao jambo ambalo sio sawa na baadaye ndoa hiyo huishia kwenye uzee wenye uchungu na upweke mkubwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

mwanga wetu maoni