mwenga wetu
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo(chadema), mkoa wa Arusha “kimewapiga stop”
wanachama wake, kutangaza nia ya kugombea ubunge katika majimbo matatu,
yanayoshikiliwa na wabunge wa chama hicho,hadi hapo Bunge litakapovunjwa
rasmi julai 2 mwaka huu.
Majimbo
hayo ni jimbo la Arusha mjini, mbunge wake, Godbless Lema, Jimbo la
Arumeru Mashariki, mbunge Joshua Nassari na Jimbo la Karatu mbunge,
Mchungaji Israel Natse ambapo tayari kuna wanachama wa chama hicho,
wameanza kutangaza nia za kuwang’oa wabunge hao.
Akizungumza
na mwananchi leo, Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro
alisema, maagizo anayoyatoa ni kutekeleza utaratibu ambao umetolewa na
Kamati Kuu ya chama hicho,kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao.
“Naomba
hapa ieleweke kuwa hatuzuwii mtu kugombea lakini tunataka afuate
taratibu ili kuzuia vurugu na kama mtu akikiuka sasa ina maana atakuwa
amepoteza sifa”alisema Lazaro.
Lazaro
alisema nia ya agizo hilo ni kuondoa vurugu na mpasuko ndani ya chama
kabla ya wakati muafaka wa kutangaza nia na kuanza kampeni haujafika,
lakini kwa majimbo yaliyo na wabunge wa CCM, wagombea wanaruhusiwa
kutangaza nia.
Alisema
chama hicho, kitatoa ratiba ya uchaguzi karibuni na fomu za
kugombea nafasi mbali mbali zitapatikana katika ofisi za chama hicho,
katika ngazi zote ila kwa maeneo yenye wabunge na madiwani wa chadema,
fomu zitapokelewa bila kutangaza nia na kuanza kampeni.
Tamko
hilo limekuja kukiwa na mpasuko mkubwa ndani ya Chadema katika majimbo
hayo matatu, kutokana na idadi kubwa ya makada wa chama hicho, kuanza
kunyemelea majimbo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni