Kumekuwa
na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha
Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu
kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.
Kumesambazwa
picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo
hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na
Mamlaka ya nchi. Lowassa Amesema hajui na wala ahusiki na usambazaji wa
Noti hiyo Mitandaoni
Mhe.
Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii,
lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao
kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo
yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni