Bwana
Zimbo (kwenye picha), alikuwa hajaajiliwa kupata kazi tangu alipomaliza
chuo, na alishika nafasi ya kwanza kabisa kitaifa katika University of
Port Harcourt alipokuwa akichukua degree ya pili.
Alikuwa anahangaika huku akijaribu kumuhudumia mama ya aliyekuwa anateseka kwa ugonjwa wa Kansa ya Ziwa.
Siku
kadhaa zilizopita alienda kutafuta dawa katika duka lililo mbali na
alipokuwa akiishi ambapo alienda kumtafutia dawa mama yake aliyekuwa
anateseka na maumivu ya gonjwa lililokuwa likimsumbua.
Bwana Zimbo
alifika dukani na kumkosa mtoa huduma wa duka hilo la dawa ndipo
alipofikiria na kuona mama yake anateseka basi akaamua kuingia na
kuchukua dawa zenye thamani ya shilingi elfu 9 tu na kuiacha pesa hiyo
dukani humo humo.
Baada ya kumaliza kuchukua dawa na kuacha hela
ndani alianza kutoka nje akikimbia kuwahisha dawa kwa mama ndipo mtu wa
duka la dawa alitokea pembeni na kuanza kupiga kelele za,
"mwizi,mwizi,mwiziii...."
Bwana Zimbo alizungukwa na wananchi wenye
hasira kali ambao walianza kushusha kipigo kikali bila hata kuuliza
mwisho wa siku wakamuwekea tairi la gari shingoni na kumpiga moto mpaka
akafa, lakini kabla hajafa kuna jamaa alichukua simu ya Bwana Zimbo na
kuiweka mfukoni, ilipokuwa mfukoni ziliingia ujumbe mbili kwenye simu ya
bwana Zimbo. moja ikisema "wahisha dawa mama yako amezidiwa sana na
amekata kauli fanya uje na usafiri tumuwahishe hospitali"
ujumbe
wa pili ulikuwa unasema. "Bwana Zimbo umechaguliwa kuwa Meneja katika
kampuni yetu ya mafuta na kazi itaaza siku ya kesho kutwa fanya uje
uweze kumalizia taratibu za mwisho uwe kazini".
Hayakupita hata masaa mawili na mama yake Zimbo na ye alipoteza maisha.
Dunia
gani hii machozi hayakujificha baada ya kusoma hii kijana amekufa
wakati akijalibu kusaidia maisha ya mama ya ke mzazi ambaye naye alikufa
kwa kuchelewesha hospital na anakufa akiwa amepata kazi na kupewa
nafasi ya juu kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni