Kufuatia
baadhi ya wasanii wa Bongo Movies na mmoja wa Bongo Flava kutangaza
kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi huko Mbeya katika Maanzimisho ya
miaka 37 ya chama hicho.
Kumekuepo
na mawazo tofauti kuhusu uamuzi waliochokua wasanii hao. Wengine
wakisema kua wasanii hao wamepewa mshiko ili waipaishe CCM wengine
wakisema kua walichofanya ni jambo zuri.
Leo
msanii Bob Junior kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliamua kuwachana
wasanii waliojiunga na CCM, alisema kua hakukua na ulazima wa wao
kujiingiza katika siasa na pia alisisitiza kua hakukua na ulazima wa wao
kujitangaza kua wameiunga na chama hicho. Moja ya kauli aliyoisema ni "muelewe
kwamba iyo ni janja ya nyani kwani sio kuingia kila sehem mpaka watu
wajue bongomoves so mjipange kwan mtaanguka kisanaa "
Itakumbukwa
kua mwaka 2010 mwanadada Nakaya na msanii Marlow walijiingiza katika
siasa jambo ambalo lililowafanya kushuka kimziki hadi leo hawasikiki.
Msanii Marlow kupitia gazeti moja alisema kua anajutia kitendo chake cha
kujiingiza katika siasa kwani kilimshusha sana kisanaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni