Stori: Makongoro Oging’
WANASEMA
za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka
huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35)
kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Hussein Shaban akiwa amevuliwa nguo na kupewa kichapo baada ya fumanizi.
Sakata
hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi, Tegeta kwa
kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mke wa kigogo huyo
ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
CHANZO CHA FUMANIZI, KUTOWEKA AMANI
Akisimulia
tukio zima mwanzo hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini, alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani
ya ndoa yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake
kupoteza amani, mke alibadilika tabia ghafla.
Bwana Hussein akitembezwa mitaani.
“Siku
moja nilikuwa natafuta nyaraka za kazini ambazo nilikuwa nimeziweka
kwenye begi la kubebea kompyuta mpakato (laptop), lakini sikuzikuta.
“Niligundua vitu vyangu vingi havipo ndani kama vile mashati, suruali, redio ndogo na saa ya ukutani. Nilimuuliza mke wangu akanipa majibu rahisi.
UCHUNGUZI WA KINA WAANZA
“Nilianza
uchunguzi, niliwahoji shambaboi wangu kuhusu tabia ya mke wangu ambapo
waliniambia kila siku nikitoka kwenda kazini nyuma kuna mtu huingia
nyumbani kwangu na kukaa na mke wangu kwa muda mrefu ndani.
“Kwa
kidokezo hicho, siku moja nilichukua simu ya mke wangu ya kijanjani,
nikaipekua na kugundua namba moja ambayo amekuwa akiwasiliana nayo mara
kwa mara. Hii namba aliisevu kwa jina la Mwajuma Jumanne.
...Wananchi wakimpiga picha Hussein aliyefumaniwa na mke wa mtu.
“Ajabu
ni kwamba, kwa namba hii nilikuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wa
mapenzi kati ya mke wangu na huyo Mwajuma Jumanne. Nilianza kuhisi kuna
jambo.
“Moja
ya meseji ilisema yeye (Mwajuma) hana mke! Nikajua huyo Mwajuma ni
mwanaume niliyeambiwa na shambaboi kuwa huwa anakuja nyumbani kwangu.
“Pia upelelezi wangu uligundua kuwa mwanaume huyo ama huwa anamuibia vitu mke wangu au alikuwa anapewa.
“Niliwahi
kuambiwa kuwa kuna siku mke wangu alimpa mwanaume huyo shilingi elfu
sitini (60,000/) na akarudia tena hivi karibuni kumpa kiasi hichohicho,”
alisema kiongozi huyo.
Hussein akijikinga sehemu za kichwa wakati akipewa kichapo na wananchi.
POLISI WAPEWA TAARIFA
Alisema
kufuatia mambo yote hayo, aliamua kwenda Kituo cha Polisi Wazo, Dar
kutoa taarifa ya kupotelewa na vitu akimtaja mwanaume huyo kwamba ndiye
anayemtuhumu. Kwa ujasiri mkubwa, kiongozi huyo aliwaambia polisi kwamba
mtu huyo angemtafuta mwenyewe, likafunguliwa jalada namba
WP/RB//7720/2013 WIZI.
MUME AANDAA SAFARI YA UONGO
Akiendelea kusimulia mkasa huo, kiongozi huyo anasema:
“Siku
ya tukio, nilijifanya nasafiri kwenda Dodoma kikazi ili kumpa mwanya
mgoni wangu kujitawala, niliondoka nyumbani alfajiri huku nikiwa
nimeweka wapelelezi wangu.
“Ilipofika
saa tano asubuhi, Hussein aliingia nyumbani kwangu na kuanza kujimwaga
kama kwake bila kujua arobaini yake ilikuwa inatimia siku hiyo.
..akizidi kutembezwa mtaani.
FUMANIZI LATIMIA
“Mimi na wapelelezi wangu tulivamia nyumba, tukagonga mlango, mke wangu akafungua. Aliponiona ni mimi alianguka kwa kiwewe.
“Nilichungulia
ndani kupitia dirishani nikamwona mgoni wangu akivaa shati. Alitoka
mbio kuelekea getini. Nilichomoa bastola na kupiga risasi moja hewani,
ikampagawisha, akataka kupanda ukuta.
“Nilipiga
filimbi watu wakaja, walipojua kisa, walimvua suruali na kuanza kumpa
kipigo huku wakimtembeza mpaka moja ya sehemu anazofanyia biashara zake
za kuchemsha supu na kukaanga chipsi, bahati yake aliokolewa na polisi,”
alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”
Hussein akiwa ndani ya gari la polisi waliofika kumnusuru.
KAKA WA MTUHUMIWA
Kaka
wa damu wa Hussein aliyejitambulisha kwa jina la Tambwe alisema kitendo
alichokifanya mdogo wake ni cha aibu ila anapinga adhabu aliyopewa ya
kutembezwa uchi.
“Hili
tukio alilofanya mdogo wangu ni baya, hata baba yetu mdogo hapa mjini
siwezi kumwambia kwa sababu linaweza kumpa presha,” alisema mtu huyo
ambaye alimuwekea dhamana polisi mgoni huyo.
Kaka
mwingine wa mtuhumiwa, Hamis alisema mama yao mzazi (hakumtaja jina) na
bibi yao waliopo Tabora walizimia baada ya kusikia tukio hilo na
wameongea kwa simu na mtendewa ili amsamehe mgoni wake.
MKE WA MTUHUMIWA
Mke
wa mtuhumiwa, Pili Muhammed akizungumzia fumanizi la mumewe kwa njia ya
simu akiwa Rufiji, Pwani alisema: “Mume wangu si mkweli katika mapenzi
yetu tangu siku nyingi ila niliamua kuvumilia nikiamini atabadilika
lakini badala yake sasa amekamatwa ugoni.”
Aliongeza:
“Siku ya tukio mtoto wetu mchanga alikuwa anaumwa, nilipomuomba mume
wangu anisindikize hospitali aliniambia hajisikii vizuri, akabaki
nyumbani kulinda nyumba.
“Niliporudi
sikumkuta na mpaka giza linaingia hakurejea, baada ya muda kidogo
nikaambiwa amekamatwa ugoni yupo Kituo cha Polisi Tegeta (si Wazo).
Ndiyo nikawapigia simu kaka zake wakaenda
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni