Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul
alihudhuria
harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali
mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.
Awali
kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua
mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo
iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja afrika, Aliko Dangote.
Blogs
hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu
ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha
wengi kumponda.
Akihojiwa
na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo
iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za
dimond kuhudhuria katika harusi yake.
Okoye
alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix
Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha
kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?
Kushangaa
huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya
harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia
viuno vya ngololo ni nani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni