IMEBAINIKA kuwa Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi.
Akizungumzia
ishu hiyo wakati wa uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Arumeru
jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikemea
vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku akisisitiza kula sahani moja
na wahusika.
Kamanda
huyo aliwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa
kutoa taarifa mara moja wanapogundua uhalifu wa aina hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni