Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema
kuwa anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015,
kutokana na kuwapo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM, wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.
Makamba
ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM alisema: “Kwanza
ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana
walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu
wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi
kugombea kwa muda sasa.”
Aliongeza:
“Mwanzoni sikuona uzito sana, yaani sikuzingatia sana, lakini kwa
kadiri siku zinavyokwenda ni kwamba ushawishi umekuwa mkubwa na hivyo
niseme ni jambo ambalo sasa ninalitafakari kwa kina”.
Alisema
ikiwa ataamua kuwania urais, atafanya hivyo wakati mwafaka kwa
kuzingatia utaratibu utakaowekwa na chama hicho, lakini akasema kwa sasa
si wakati wake. Makamba alikuwa akijibu hoja za gazeti hili lililotaka
ufafanuzi wake kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba ameanza harakati za
kuusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Gazeti
hili lilidokezwa kuwa hatua yake hiyo imemwingiza katika mvutano usio
rasmi na wanasiasa ambao tayari wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo
ya juu ya uongozi nchini, wakiwamo wale wa kambi ya urais aliyokuwa
akidaiwa kuwa mmoja wao.
Awali
iliaminika kuwa Makamba alikuwa katika kambi ya Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, lakini wachambuzi wa masuala ya kisisa wanasema ‘katika
siku za karibuni mwenendo wake unaashiria kwamba si mmoja wa wanaomuunga
mkono kiongozi huyo, bali ni mtu mwenye mipango yake binafsi ya
kisiasa”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni