Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 31 Oktoba 2013

RAIS WA FIFA ATAKIWA KUMUOMBA MSAMAHA RONALD

Real Madrid imeliandikia barua shirikisho la soka duniani FIFA likimtaka Sepp Blatter kuomnba radhi kufuatia maoni yake aliyoyatoa kuhusu Cristiano Ronaldo ndani ya hotuba yake kwa muungano wa wanafunzi wa Oxford  (Oxford Students Union).
Ndani ya mazungumzo yake Blatter alisikika anadhani kwa upande wake anadhani Lionel Messi, lakini pia akisimama kutoka kitini kwa kujaribu kutoa maelezo kwa mfano huelekeza maelezo kwa upande wa Ronaldo.

Blatter ni kama alikuwa akimchimba mshambuliaji wa Madrid akisema kuwa 
'Mmoja ana matumizi makubwa kwa ajili ya nywele zake kuliko mwingine'.
Katika mkutano wake na wanahabari kuelekea katikam mchezo wa kesho Jumatano dhidi ya Sevilla, kocha wa Madrid Carlo Ancelotti amenukuliwa akisema 

'Rais Florentino Perez wa klabu yangu ametuma barua FIFA akitaka ufafanuzi juu ya maoni hayo ambayo aymeonyesha juu ya kukosa heshima kwa Cristiano.'

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

mwanga wetu maoni