1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
» Zawadi ni moja ya sehemu husika katika Mapenzi inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye kupendezasiku zote, faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa zawadi na kila anaepewa zawadi siku zote hujihisi kama ni mtu anaependwa na
anaejaliwa na kuthaminiwa hususani katika
ulimwengu wa Mapenzi unapompa mpenzi wako zawadi basi faham ya kwamba
utamfanya mpenzi wako ajione kama ni wapekee kwako na anathamani kubwa
kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi yake kwako, kikubwa zingatia
pindi unaponunua zawadi kwa ajili ya kumpa mpenzi wako jitahidi kuwa
mbunifu na uwe ni mwenye kubadilika sio kila siku zawadi zile zile
zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa mpenzi wako kuwa mbunifu na jaribu
kumpa mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano kama Card, maua, nguo
n.k. Utamfanya azidi kukupenda zaidi na zaidi.
2. MSIFIE MPENZI WAKO:
»
Sifa zinaleta changamoto katika mapenzi. Unapaswa kutambua kuwa usiwe
mchoyo wa sifa kwa mpenzi wako usisubiri watu wapembeni wamsifie mpenzi
wako pindi anapofanya jambo zuri na lenye kupendeza chukua nafasi hii
wewe kama kioo chake unadhani usipo msifia mwenza wako unataka nani
amsifie?! Jitahidi kudhihirisha sifa kwa mpenzi wako kwa mfano umemuona
mpenzi wako kapendeza basi usisite kumwambia "Sweetie nimependa vazi
lako la leo ama hakika umetoka sex nakutamani zaidi ya siku zote
navyokutamani ingawa siku zote unaziteka hisia zangu ila leo ni zaidi"
unaweza kumpa maneno kama haya na mengine mazuri ya kuvutia, sifa zipo
nyingi mbali na kumsifu mavazi yake hata tabia n.k. Kwa kufanya hivi
utamfanya mpenzi wako azidishe mapenzi kwako kwani atahisi kampata mtu
anaejali ubora na uhalisia wake kimaumbile na kimatendo. ZINGATIA:-
Usitoe sifa ilimradi sifa zisizo na ukweli.
3. EPUKA KUMUUDHI MPENZI WAKO:
»
Sote tunafahamu kuwa hakuna binadamu aliekamilika na hakuna alietolewa
nyongo kila mtu anakasirika na anakosea ila solution kubwa ni kudhibiti
hasira na kurekebisha makosa na kusuluhisha hususani kwenye mapenzi,
katika mapenzi hakuna jambo baya linalopunguza upendo kama ugomvi na
kumuudhi mpenzi wako mara kwa mara. Ili kuboresha mapenzi na kulifanya
penzi lako liwe imara na lenye kuvutia basi jitahidi kuepuka kumuudhi
mpenzi wako na pindi ikitokea umekorofishana na mpenzi wako jaribu
kutafuta suluhu mwite kaa nae muombe samahani iwapo kama unakosa na hata
ikitokea kosa si lako pengine kakuudhi na bado unamuhitaji usikae na
kinyongo wala usiumize nafsi yako kaeni muyamalize muendeleze mahusiano
yenu na msiwe watu wa kuzungumzia tofauti zenu kwa watu wa pembeni. Kwa
kufanya hivi daima mtakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na mapenzi yenu
hayatofika kikomo zaidi yataendelea kushamiri.
4. MFANYIE YATAKAYO MFURAHISHA:
»
Kuna mambo mengi mazuri na yakuvutia katika mapenzi unaweza kuyafanya
kwa mpenzi wako yakamfurahisha kwa mfano unaweza kusoma tabia ya mpenzi
wako na ukajua ni nini anapenda na kipi hapendi kufanyiwa ukajitahidi
kujilinda kumtendea asiyoyapenda na ukaufungua moyo wako kwa kumridhisha
kumfanyia kile anachokipenda. Katika mapenzi watu wengi hupenda
kutolewa Out, kupewa ofa ya lanch, kupewa zawadi zenye mvuto na zenye
hamasa nzuri kwenye mapenzi. Unaweza kufanya vitu vizuri vyenye kuvutia
kwa mpenzi wako vikamvutia ikawa ni nafasi nzuri kwako kumfanya azidishe
mapenzi.
5. KUWA MTU WA UTANI KWAKE:
»
mpenzi msomaji ninapozingumzia mapenzi na maanisha mazoea
yaliyoambatana na upendo, siku zote mapenzi hujijenga moyoni kwa mtu
kutokana na ukaribu na mazoea yaliyopo baina ya watu wawili, katika
pointi hii ya mwisho nataka nizungumzie utani katika mapenzi unafaida
gani. Mpenzi msomaji fahamu yakuwa utani ni moja ya sehemu katika
mapenzi na utani unasaidia kuboresha mapenzi ila utani ninaotaka
kuuzungumzia hapa ni utani wa kawaida na sio ule wa kuvuka mipaka. Elewa
wazi kabisa unapokuwa na mpenzi wako na ukawa ni mtu wa utani
inakusaidia wewe kumfanya mpenzi wako akuzoee na awe anajisikia kuwa
karibu nawewe muda wote kwani utakuwa unamfurahisha kutokana na utani
wako. ZINGATIA:- Usivuke mipaka ya utani, usimtanie kupitiliza, mtanie
kutokana na mazingira, usiwe utani unaofanana nakweli, mtanie kwa
faida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni