WANA WAKE NCHINI SAUDI WAPANGA KUANDAMANA KUPINGA WAO KUNYIMWA KUENDESHA GARI

Leo
October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana
kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni
nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama
wanaweza.
Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia
zimewaonya Wanawake hao kutoandamana katika maandamano hayo yatakayokua
ya aina yake na ya tatu kutokea nchini humo toka mwaka 1990 ambapo
Wanawake kadhaa walikamatwa na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo
linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote ambae amepanga kuendesha gari.
Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo
atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana
ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao
wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa
hawajakamatwa.
Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17 wamesain kura ya
ndio itakayo waruhusu Wanawake wa Saudi kuendesha magari ambapo pia
idadi ya Wanaume wanaosupport imeendelea kuongezeka kwa
kasi.SOURCE..DIKODIKO NYAGALE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni