MSANI WA TABORA LIZZ DADY ACHEMSHA FIESTA SUPER NYOTA 2013
LIZZ DADY | Mshindi super nyota fiesta 2013 Tabora [PICHA HAIHUSIANI NA TUKIO]
Msanii huyu ameuambia mtandao huu kuwa upatikanaji wa mshindi haumpi tu
wasiwasi ila hakuna chochote walichokifanya kumpata mshindi huyo wa
SUPER NYOTA ambapo Liz Dady amedai kuwa hata mashabiki waliona na
kutambua ushindi kuwa haukustahili kwenda hata kwa huyo mshindi wa
kwanza na wapili. Akijigusia yeye mwenyewe, amesema hata kama
hakustahili kuwa yeye lakini si kwa ushindi walioutoa kwa mshindi
waliyempanga wao.
"Mimi niling'ara jukwaani kiasi cha
mashabiki kunitaka nirudi jukwaani, si mimi tu niliyetisha kwa jukwaa
ila pia jamaa mmoja wa Shinyanga pia aling'ang'aniwa na mashabiki kwa
uwezo alouonesha.... kupitia mengi yaliyojiri pale yalinifanya niaamini
kuwa mshindi amepangwa, sikatai kushindwa lakini mziki hauendi hivyo
kwani mwisho mashabiki ndio watakao zisikiliza kazi zao na kama
watazirusha hizo battle radioni utapata nguvu ya kujua ninachokiongea na
utaweza kukijaji" Alisema Liz Dady
Mashindano hayo yamefanyika
jana usiku tarehe 25/10/2013 club sansiro jijini dar. Kinachouma kama
kweli wamechakachua, je mziki utaendelea kweli?
asikate tamaa
JibuFuta