Sakata la
vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua
sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana
walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa
katika nchi husika.
Akizungumza na gazeti hili, Zitto
alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha
wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.
Alibainisha kuwa tangu kuibuka kwa
sakata hilo mwaka 2012 na Bunge kuiagiza Serikali kufuatilia, Serikali
haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi kuhusu Watanzania waliohifadhi
fedha nchini humo.
“Jana nilikutana na Waziri wa Fedha
na akatuacha na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa,
Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi
(Multilateral convention on administrative assistance in tax matters),”
alisema Zitto na kuongeza;
“Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima
haki ya kupata taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha
huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania
popote anapopata kipato halali lazima alipe kodi.”
Zitto alieleza kuwa kitendo cha
Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa
taarifa za benki za watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo
Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi
au la.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni