Siku
za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi zisizo rasmi kuwa mastaa wawili wa
filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya hawana
maelewano
mazuri chanzo kikidaiwa ni Irene Uwoya kutaka kumpoteza Batuli kwenye
tasnia ya filamu ili asifurukute. Habari hizo zinaenda mbali zaidi
zikidai kuwa kuna kipindi Batuli alikuwa anaumwa maeneo ya kifuani
lakini baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wakiamini Uwoya ndiye
kamfanyia mambo ya kilozi(ushirikina).
Tetesi
hizo tulizipuuza mwanzoni lakini zinaonekana kurudi tena kwa kasi hivyo
tuliamua kuwatafuta mastaa hao wawili ili watoe ufafanuzi wao wenyewe
na wa kwanza kuulizwa alikuwa Uwoya hata hivyo namba yake ilionekana
kutokuwa hewani alipotafutwa juzi na jana alipotumiwa ujumbe namba yake
ilionekana bado haipo hewani. Batuli nae alitumiwa ujumbe juzi kuhusu
issue hiyo lakini hakujibu mpaka jana usiku ndiyo alijibu akisema
alikuwa busy sana. Batuli alisema "sina ubaya na msanii yeyote na moyo
wangu ni mweupe na nina mapenzi na wasanii wenzangu wote, nawapenda sana
anayeniwinda kwa ubaya Mungu atanipa ulinzi wake, sipendi uadui na mtu
namuachia Mungu atanilipia yote"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni