Kocha wa
zamani wa Manchester United, Alex Ferguson amesema atampa ushirikiano wa
kutosha kocha wa sasa wa Manchester United, David Moyes.
Ferguson alisema hayo wakati
alipokuwa akizindua kitabu chake ambacho kimewakosoa nyota wengi
aliokuwa nao Manchester United kama Roy Keane, David Beckham, Wayne
Rooney, Carlos Tevez na Anderson.
“Mimi nilipojiunga Manchester United
nilipewa ushirikiano wa kutosha na Matt Busby, alinisaidia sana,
ninatarajia kumsaidia David Moyes kama mimi nilivyosaidiwa na Busby,”
alisema Ferguson.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu msimu
huu kocha Moyes alisema ratiba siyo nzuri kwa upande wa Man U kwani
katika mechi zake tano za mwanzo ilipangiwa kucheza na Chelsea,
Liverpool na Manchester City. Akizungumzia hilo kocha Ferguson
alisema,”hata mimi nilipoiona ratiba ya msimu huu niliona Manchester
itakuwa na wakati mgumu mwanzoni mwa msimu.”
Alisema,”Hata hivyo watu wengi wanasahau Man U ni timu ambayo inaweza kutoka chini na kupanda mpaka juu na kutwaa ubingwa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni