Idara
ya polisi nchini Kenya imesema kuwa polisi watano na raia wawili
wameuawa katika shambulio dhidi yao kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.
Polisi wengine wawili hawajulikani waliko.
Shambulizi
hilo lilifanyika katika barabara iliyoko kati ya kambi kubwa zaidi ya
wakimbizi duniani ya Dadaab na mji wa Mashariki wa Liboi.
Polisi hao waliuawa wakiwa wanashika doria wakati gari lao liliposhambuliwa kwa risasi.
Mpaka
wa Kenya na Somalia umekuwa kitovu cha mashambulizi ya kuvizia
yanayofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab pamoja
na makundi mengine ya watu waliojihami.
Mashambulizi ya mara kwa mara hufanyika kwenye mpaka huo ingawa haijulikani nani aliyehusika na shambulizi la leo.
Wanamgambo
wa Al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi Kenya na la hivi karibuni
likiwa lile lililofanywa dhidi ya jengo la maduka la Westgate mjini
Nairobi ambapo waliwateka watu nyara na kuwaua wengine mwezi Septemba.
Watu 61 waliuawa na wengine miambili kujeruhiwa vibaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni