Wachezaji
wa Simba SC, Haruna Shamte (kushoto) na Joseph Owino wakijadiliana
jambo baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Coastal Union jana kwenye Uwanja wa
Mkwakwani mkoani Tanga. (Picha na Richard Bukos / GPL,TANGA).
Yanga
SC jana imeweka kimbindoni pointi tatu baada ya kuichabanga mabao 3 - 0
timu ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao
ya Yanga yamefungwa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili katika dakika ya
12 na 81 wakati lingine likifungwa na Frank Domayo mnamo dakika ya 72.
Wakati
Yanga wakitoka vifua mbele leo, watani wao Simba SC wao wameshikwa
sharubu baada ya kulazimishwa sare ya 0 - 0 na Coastal Union ya mkoani
Tanga. Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
mwanga wetu maoni